Tuesday, 10 November 2015

Maombi ya Baadhi ya Wasomaji Wetu kuhusu kufahamu Msimu wa Tangawizi



 
Asante wasomaji wa mtandao wetu, huku mkitaka kufahamu zaidi msimu wa Tangawizi katika kata yetu ya Lumbiji. Tangawizi ni zao lilnalopatikana sana hapa Lumbiji hasa katika kipindi cha mwezi wa NANE hadi wa KUMI na Mwanzoni mwa Mwezi wa KUMI na MOJA. Na bei ya zao hili hutofautiana kila msimu mpya. Kufahamu Bei yake kwa msimu husika usisite kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano yetu yaliowekwa hapa mtandaoni.
Share:

Saturday, 31 October 2015

Matokeo ya DARASA la Saba 2015- KATA YA LUMBIJI

SHULE YA MSINGI LUMBIJI>>><<BONYEZA HAPA>>

SHULE YA MSINGI KISONGWE>> <<BONYEZA HAPA>>

SHULE YA MSINGI KISALE>> <<BONYEZA HAPA>>

Share:

Friday, 3 July 2015

Habari: Lumbiji Sekondari yatoa mwanafunzi mmoja wa kwenda kidato cha Tano 2015

Habari Wadau wa Lumbiji, Shule ya sekondari lumbiji imefanikiwa kutoa mwanafunzi mmoja kujiunga na kidato cha tano 2015. Hii imeonekana kama ni mafanikio kwa shule yetu kwani ndio inaanza kabisa. Kwa mara ya kwanza imeanza kutoa wanafunzi wa kidato cha nne 2013 ikiwa na jumla ya wahitimu 4 tu ambapo kutokana na sababu mbalimbali watoto wawili matokeo yao hayakutoka. Kwa mwaka 2014 kulikuwa na jumla ya wahitimu 9 na kufaulisha wanafunzi 8 na mmoja kwa bahati mbaya alifeli katika daraja la sifuri.

Kutokana na matokeo hayo shule ya sekondari Lumbiji imefanikiwa kutoa mwanafunzi mmoja ambaye amechaguliwa na TAMISEMI kujiunga na shule ya sekondari Dr. Nchimbi iliyopo Songea Ruvuma.

NAMBA YA MTAHINIWA-JINA-JINSI-SHULE ATOKAYO-SHULE AENDAYO-MCHEPUO-MKOA-WILAYA
S4435/0007 -MUSA RAMADHANI-M-       LUMBIJI-              DR NCHIMBI   -     HKL-RUVUMA-SONGEA (M)

Shule ina Jumla ya walimu 6 wa masomo ya sanaa yanayofanana zaidi hivyo kufanya mchakato wa ufundishwaji wa masomo mengine inakuwa vigumu. Hata hivyo kwa mwaka huu wa masomo shule imeletewa baadhi ya walimu wakiwemo wa masomo ya sayansi yaani Kemia, Fizikia na Hisabati, hivyo tuna matumaini kwa mwaka ujao kuwa wa mafanikio zaidi.

Katika matokeo haya kulikuwepo na changamoto zifuatazo:-

1. Ukosefu wa walimu hasa wa Sayansi na baadhi ya masomo mengine ya sanaa.

2. Mazingira ya Kusomea ni tatizo kwani hakuna maktaba ya kusomea wala hata hakuna hata chumba cha ziada kwaajili ya kujisomea.

3. Ukosefu wa Madarasa. Shule ya sekondari Lumbiji inakumbwa sana na changamoto ya kutokuwepo na vyumba vya kutosha vya madarasa. Ingawa tunashukuru Serikali kusisitiza kujitolea kwa wananchi kuongeza vyumba vya madarasa.

4. Muamko wa kusoma. Kutokana na mazingira yalivyo Kuna changamoto ya watoto wetu wa kutokuwa na muamko wa kusoma badala yake wengi huishia kuacha masomo.

5. Tatizo la hosteli. Hili ndilo tatizo kubwa sana, kwani katika eneo la shule hakuna huduma ya hosteli ya shule wala ya mtu binafsi. Hivyo wanafunzi wanatoka maeneo ya mbali isitoshe ukizingatia kuwa kuna kupanda na kushuka milima baadhi ya maeneo. Kutokana na sababu hii kuna baadhi ya wanafunzi wanaamua kupanga mitaani na inapofikia kwamba kuna maisha magumu, mwanafunzi anaamua kurudi nyumbani kabisa kupumzika. ITAENDELEA.....
Share:

Saturday, 14 February 2015

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014-SHULE YA SEKONDARI LUMBIJI

Share:

Saturday, 17 January 2015

Matokeo ya kidato cha pili shule ya Sekondari Lumbiji 2014



 
TAZAMA MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA PILI SHULE YA SEKONDARI LUMBIJI



CHANZO: NECTA

Share:

Friday, 16 January 2015

Picha: Mradi wa maji uliyofika shule ya sekondari Lumbiji na eneo lote la Mzingwi

 Tenki linalohifadhi maji, Lipo eneo la Kanisa Lumbiji
 Baadhi ya Wananchi walionufaika na mradi huo, wakitchota maji

Picha zote na Lumbiji Yetu Blog
Share:

Popular Posts

Copyright © LUMBIJI KWETU | Powered by Blogger Design by Yuvinusm