Habari Wadau wa Lumbiji, Shule ya sekondari lumbiji imefanikiwa kutoa mwanafunzi mmoja kujiunga na kidato cha tano 2015. Hii imeonekana kama ni mafanikio kwa shule yetu kwani ndio inaanza kabisa. Kwa mara ya kwanza imeanza kutoa wanafunzi wa kidato cha nne 2013 ikiwa na jumla ya wahitimu 4 tu ambapo kutokana na sababu mbalimbali watoto wawili matokeo yao hayakutoka. Kwa mwaka 2014 kulikuwa na jumla ya wahitimu 9 na kufaulisha wanafunzi 8 na mmoja kwa bahati mbaya alifeli katika daraja la sifuri.
Kutokana na matokeo hayo shule ya sekondari Lumbiji imefanikiwa kutoa mwanafunzi mmoja ambaye amechaguliwa na TAMISEMI kujiunga na shule ya sekondari Dr. Nchimbi iliyopo Songea Ruvuma.
| NAMBA YA MTAHINIWA- | JINA | -JINSI | -SHULE ATOKAYO- | SHULE AENDAYO | -MCHEPUO | -MKOA- | WILAYA |
| S4435/0007 | -MUSA RAMADHANI- | M- | LUMBIJI | - DR NCHIMBI | - HKL | -RUVUMA- | SONGEA (M) |
Shule ina Jumla ya walimu 6 wa masomo ya sanaa yanayofanana zaidi hivyo kufanya mchakato wa ufundishwaji wa masomo mengine inakuwa vigumu. Hata hivyo kwa mwaka huu wa masomo shule imeletewa baadhi ya walimu wakiwemo wa masomo ya sayansi yaani Kemia, Fizikia na Hisabati, hivyo tuna matumaini kwa mwaka ujao kuwa wa mafanikio zaidi.
Katika matokeo haya kulikuwepo na changamoto zifuatazo:-
1. Ukosefu wa walimu hasa wa Sayansi na baadhi ya masomo mengine ya sanaa.
2. Mazingira ya Kusomea ni tatizo kwani hakuna maktaba ya kusomea wala hata hakuna hata chumba cha ziada kwaajili ya kujisomea.
3. Ukosefu wa Madarasa. Shule ya sekondari Lumbiji inakumbwa sana na changamoto ya kutokuwepo na vyumba vya kutosha vya madarasa. Ingawa tunashukuru Serikali kusisitiza kujitolea kwa wananchi kuongeza vyumba vya madarasa.
4. Muamko wa kusoma. Kutokana na mazingira yalivyo Kuna changamoto ya watoto wetu wa kutokuwa na muamko wa kusoma badala yake wengi huishia kuacha masomo.
5. Tatizo la hosteli. Hili ndilo tatizo kubwa sana, kwani katika eneo la shule hakuna huduma ya hosteli ya shule wala ya mtu binafsi. Hivyo wanafunzi wanatoka maeneo ya mbali isitoshe ukizingatia kuwa kuna kupanda na kushuka milima baadhi ya maeneo. Kutokana na sababu hii kuna baadhi ya wanafunzi wanaamua kupanga mitaani na inapofikia kwamba kuna maisha magumu, mwanafunzi anaamua kurudi nyumbani kabisa kupumzika. ITAENDELEA.....
0 comments:
Post a Comment