Sunday, 22 September 2013

Wakulima acheni kulima kwa mazoea, asema ofisa

 
Morogoro. Imeelezwa kuwa baadhi ya wakulima wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, wamekuwa waoga kutumia mbinu mpya za kilimo na badala yake, wanaendelea kulima kilimo cha mazoea na kisichokuwa na tija.
Hayo yameelezwa na Ofisa Kilimo wa Shirika la Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania, Ernest Jerome, alipokuwa akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Kisongwe katika Kata ya Lumbiji.
Jerome ambaye pia ni Meneja wa Mradi wa Rafiki wa Mazingira, amesema wameanzisha shamba darasa la wakulima 30, ili litumike katika kuwafundishia wakulima mbinu bora za kilimo.
Alisema mbinu hizo ni pamoja na zile zinazolinda mazingira na zinazowawezesha wakulima kuvuna mazao mengi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo, aliwataka wakulima kutowasikiliza watu wanaopotosha na badala yake , wafuate mafunzo ya wataalamu.

Gazeti la mwananchi julai 22,2013

Share:

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © LUMBIJI KWETU | Powered by Blogger Design by Yuvinusm