Sunday, 8 September 2013

HUDUMA ZA JAMII

HUDUMA ZA JAMII ZINAPATIAKANA PIA

MAJI
Huduma ya maji masafi kwa wananchi yanapatikana yakutosha,kili kitongoji kinapata maji safi na yakutosha hasa katika mfumo mkuu na mzuri wa Mabomba yaliyotengenezwa kati ya mwaka 1994-95 ambapo hadi sasa huduma inaendelea na selikali inazidi kuboresha mifumo yote ya maji.

HUDUMA ZA AFYA.
Lumbiji hadi sasa ina zahanati moja inayomilikiwa na kanisa katoliki la Mt.Wilblod ambayo inatoa huduma nzuri na inatumiwa na wananchi wote wa kata ya Lumbiji.


ELIMU

Katika suala zima la elimu Lumbiji haipo nyuma kwani inazungukwa na shule:
1.Shule ya msingi Lumbiji
2.Shule ya msingi Kisongwe
3.Shule ya msingi Kisale
4.Shule ya sekondari Lumbiji

HUDUMA ZA KIROHO
Huduma hii inapatikana katika kata hii:
1.Kanisa katoriki Parokia ya Lumbiji.
2.Makanisa mengine kama Pentekoste nk
NB.Hakuna msikiti kwakuwa hakuna waumini wa dini hiyo na endapo wapo basi ni wakuja na kuondoka na wanoishi kabisa katika eneo hili bdo haijajulikana kujenga msikiti kwaajili yao.

USAFIRI
Huduma ya usafiri ipo barabara inayopitika kwa pikipiki,baiskeli na hata magari lakini hakuna usafiri wa basi,daladala n.k kwakuwa bado wadau wa usafiri hasa wamiliki wa vyombo vya usafiri hawajapeleka huduma hii.
NB.Kwa usafiri binafsi kunapitika vizuri ingawa kuna vilima kiasi.

MAWASILIANO
Huduma hii inapatikana baadhi ya maeneo na selikali inajitahidi kuboresha zaidi hsas kwenye mitandao ya simu za mkononi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © LUMBIJI KWETU | Powered by Blogger Design by Yuvinusm