Saturday, 20 December 2014

Walima maharage Kilosa kunufaika rafiki

 ZAO LA VIAZI VITAMU
Kilosa. Wakulima wadogo wa maharage katika kijiji cha Kisongwe Kata ya Lumbiji, Wilaya ya Kilosa wameanza kunufaika mafunzo ya kilimo rafiki ambacho hakitaharibu mazingira na kuwaongezea kipato katika familia.
Wakizungumzia faida wanayotarajia kuipata baada ya kupatiwa elimu ya kilimo rafiki iliyotolewa na Shirika TFCG kupitia mradi wa mabadiliko ya tabianchi,wakulima hao walisema kutokana na elimu hiyo waliyoipata wanatarajia kuendesha kilimo chenye mavuno mengi na chenye kuhifadhi mazingira.
Veronica Solomoni ambaye ni mmoja wa wakulima wa maharage alisema kabla ya elimu hiyo walikuwa wanatumia kilimo cha kuchoma moto kilichokuwa kikiharibu ardhi na kusababisha ukame, na kuiomba Serikali iwajali katika kuwapatia pembejeo za kilimo mapema ili waende sambamba na msimu wa kilimo.
Kwa upande wake Ofisa Mgharibishi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi, kupitia kilimo rafiki, Jackline Tesha na Ofisa Kilimo kutoka Mtandao wa Mjumita, Ernest Jerome walisema mradi unalenga kumsaidia mkulima mdogo kutoka katika kilimo alichonacho na kumfikisha katika kilimo cha faida ili kumkomboa na kumwongezea kipato.
Ofisa kilimo Wilaya ya Kilosa, Jonas Mboya alisema kuna changamoto nyingi wanakutana nazo katika utoaji wa elimu kwa wakulima kwa kuwa wakulima wengi hawana uelewa juu ya kilimo endelevu na kuendelea kutumia kilimo cha uchomaji moto mashamba.

chanzo: Mwananchi
Share:

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © LUMBIJI KWETU | Powered by Blogger Design by Yuvinusm