Katika mkutano au matangazo madogo yanayotangazwa mara kwa mara na serikali ya Lumbiji hasa baada ya ibada, wanawake wa Kata hii ya Lumbiji wamesisitizwa kuhudhuria kliniki hasa kipindi chote cha ujauzito. Akizungumza na wananchi Diwani wa kata ya Lumbiji mh. Hermani Msakila ikitiliwa msisitizo na Afisa mtendaji wa kata walisema kuwa kuhudhuria kliniki kwa mama mjamzito ni lazima na si la hiari. Aliendelea kusema kuwa serikali ipo kusimamia afya ya wananchi hao na kuhakikisha wanahudhuria kliniki. Hii ilitokea baada ya mama mmoja kutoka kijiji cha kisongwe hakutaka jina litajwe alipokaa nyumbani bila kuhudhuria kliniki hadi alipojifungua.
Sababu ya mama huyo kutokwenda kliniki ilibainika baada ya mda wake wa kujifungua kufika na kulazimika kupelekwa hospitali ya wilaya ya Kilosa, mama huyo alipoulizwa kwanini hakuhudhuria kliniki alidai kuwa wahudumu wa kliniki ya lumbiji walimwambia kadi ya mahudhulio ya Kliniki inauzwa kwa bei ya sh. 10,000 Kitu ambacho kilikanushwa na wahudumu wa kliniki yetu tegemezi ya Lumbiji na kuishinda kesi hiyo huku mama huyo akilalamikiwa na wananchi wa Lumbiji kuwazalilisha wahudumu. Kesi iliishia mahakamani na mama huyo kulipa faini.

0 comments:
Post a Comment