WAKULIMA
wadogo wa Kijiji cha Kisongwe, katika Kata ya Lumbiji wilayani Kilosa
wameshauriwa kuacha kuchoma mabaki na takataka za mazao katika mashamba
yao wakati wa msimu mpya wa kilimo na badala yake watumie takataka hizo
kama mbolea ili kuhifadhi na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Akizungumza
na wakulima wa Kijiji cha Kisongwe, Afisa Ugharibishaji wa Shirika
lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na mabadiliko ya tabia nchi
MJUMITA, Jackline Tesha, alisema ili wananchi hao waweze kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi ni lazima waachane na kilimo cha uharibifu. Tesha
alifafanua kwamba wakulima hao wadogo iwapo watakuwa na tabia ya
kutumia takataka zilizopo shambani kama mbolea,itasaidia kuongeza mazao
shambani na kupata mavuno ya uhakika lakini pia itakuwa inalinda
uharibifu wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment